top of page

WATEJA WA UMOJASWITCH WAIBUKA NA MAMILIONI KUPITIA BAHATI NASIBU

  • Khalidi
  • Jan 16, 2018
  • 2 min read

Kampuni ya UmojaSwitch leo imechezaesha droo yake ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo ya leo

UmojaSwitch ilianzisha bahati nasibu hiyo ya Shinda na Umoja mwezi Desemba mwaka jana kwa lengo la kutoa hamasa kwa wateja wao kupitia kampeni yao ya kubadili kadi za UmojaSwitch kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kwenye mfumo mpya wa ‘Microchip’

Afisa masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel, akichezesha bahati na sibu, kulia ni Bw Bakari Maggid Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha akishuhudia

Katika makundi matatu yaliyo chezeshwa leo kundi la kwanza limetoa washindi 25 waliojishindia T-Shirt za UmojaSwitch,

Mzunguruko wa pili umetoa washindi wa tano wa Simu za Mkononi (Smart Phone), mzunguruko wa tatu umepata washindi wawili wa fedha taslimu mara mbili ya fedha walizokuwa wanatoa kwenye Akaunt zao kupitia kadi za UmojaSwitch na Mzunguzuro wa nne umepata mshindi mmoja aliejishindia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Taslimu

Afisa masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel akizindua zozi la kuchezasha droo ya Shinda na Umojaswitch

Akiendesha Droo hiyo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bi Beatrice Emmanuel Chini ya Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid amewapongeza washindi wa zawadi hizo na kudai

kuwa watafanya mawasiliano na Benki husika wanazotumia washindi wao ili kuweza kuwapatia zawadi zao muda mchache kuanzia leo

Aidha Beaterice amewataka wateja ambao bado hawajabadilisha kadi zao za awali kufika kwenye Benki ao husika ili kubadili kadi zao na kuwea kuingia katika bahati nasibu hiyo ya Shinda na UmojaSwitch kwenye droo inayofuata.

Kampuni ya UmojaSwitch inaunganisha mabenki zaidi ya 27 Tanzania kwa lengo la kushirikiana kutoa fedha kwa njia ya kilectronic ya ATMs

Commenti


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page