top of page

MJASIRIAMALI  ATUSUA MAMILIONI YA SHINDA NA UMOJA SWITCH

  • Writer: Admin
    Admin
  • Feb 16, 2018
  • 2 min read

.

Meneja masoko Umoja Switch Beatrice Emmanuel (wapili kushoto)akipiga picha ya pamoja na washindi wa droo ya Shinda na Umoja Switch, wa kwanza kushoto ni Muhunzi kishoma, mshinidi wa mil. moja watatu kushoto ni Felista Muumbe mshindi wa Simu ya Mkononi na wa mwisho kulia ni Tarisiana Unndama mshindi wa T-shirt za Umoja Switch

Kapuni ya Umoja switch leo imewazawadia washindi wake zawadi walizoshinda kwenye droo ya pili ya Shinda na Umoja Switch iliyochezeshwa February 2 mwaka huu

Katika droo hiyo ya pili ilitoa washindi katika vipengele vinne ambavyo ni, washindi wawili wa fedha taslimu Milioni moja, mshindi wa fedha taslim mara mbili ya muamala aliyofanya kwenye ATMs za UmojaSwitch, washindi wanne wa Simu za mkononi (Smart phones) na washindi zaidi ya 20 wa T-shirt za UmojaSwitch

Akiwakabidhi zawadi hizo za afisa masoko wa Umoja Switch Umoja Beatrice Emmanuel amesema anawashukuru wateja wa Umoja Switch kwa kuendelea kutumia kadi za Umoja Switch na amewataka wale ambao hawajabadili kadi zao wafike kwenye Benki zao ili kubadilisha kadi zao na waingie kwenye droo ya Pili ya Promosheni hii ya Shinda na Umoja Switch

Meneja masoko Umoja Switch Beatrice Emmanuel (kushoto) akimkabidhi fedha Muhunzi Kisome mshindi wa mil moja droo ya Shinda na Umoja Switch baada ya kukabidhiwa kitita chake

Akizungumza na Fahari News kwa niaba ya washindi wenzake Bwana Muhunzi Kisome ambae ndio mshindi wa Milioni moja, mfanya biashara kutoka Chamanzi Jijini Dar es salaam amesema hakutegema kama angekuwa mshindi wa fedha hizo na wakati amepigiwa simu alipuuza mpaka alipoamua kujidhihirishia kwa kuangalia kama kweli kuna Droo ya Shinda na Umoja Switch inayochezeshwa kupitia Simu yake

Muhunzi Kisome mshindi wa mil moja droo ya Shinda na Umoja Switch

“kiukweli siku amini mara ya kwana mpaka nikaingia kwenye internet kuhakikisha, walivyonipigia simu mara ya pili ndo nikafika hapa na nimeamini baada ya kuona na waandishi wa habari wapo hapa, pesa yangu nitaifanyia kitu ambacho kitakua ni kukbukumbu na shukrani kwa kampuni ya UmojaSwitch” alisema Kisome

Meneja masoko Umoja Switch Beatrice Emmanuel (kushoto) akimkabidhi Felista Muumbe Simu (Smart phone) aliyoshinda kwenye droo hiyo.

Meneja masoko Umoja Switch Beatrice Emmanuel, (kushoto) Akimkabidhi Tersiana Unnduma T-shirt ya Umoja Switch aliyoshinda kwenye droo hiyo.

Kampuni ya umoja Switch imekua ikitoa huduma za kifedha kwa kushirikiana na mabemki zaidi ya 20 nchini kwa njia ya kielectronic ili kuwarahisihia wateja wa mabenki njia rahisi za kufanya miamala kwa kutumia ATMs za Umoja Switch zilizosammbaa Tanzania Nzima.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page