top of page

WAGENI WALIVYONASWA WIZI NYUMBA ZA WAGENI

  • Khalidi
  • Jan 16, 2018
  • 2 min read

Jeshi la polisi mkoani Manyara limewanasa “majambazi sugu” watatu ambao walikuwa wakiibia watu wanaolala nyumba za wageni katika miji mbalimbali.

Aidha jeshi hilo limesema jambazi mmoja ambaye alikuwa akiteka watu minadani ameuawa baada ya mapambano na polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuwa majambazi waliokuwa wakijihusisha na matukio ya wizi katika nyumba za kulala wageni ni:

Hassan Juma (40), mfanyabiashara kutoka Dar es salaam na Veronica Semu (32), mkulima kutoka Moshi.

Alisema majambazi hayo yamekuwa vinara wa kuwaibia mali zao watu wanaoingia nyumba za kulala wageni.

Alisema watu hao walikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Sedekia mjini hapa, baada ya watu kuwatilia shaka na kutoa taarifa polisi.

Alisema baada ya kupekuwa mabegi yao, polisi walikuta funguo za vitasa 71.

“Baada ya askari wangu kuwahoji wamekiri kuwa wamekua wanavunja milango au kufungua na kuiba fedha, simu, kompyuta mpakato na runinga,” alisema Kamanda Senga.

“Na hasa wamekuwa wakifanya matukio hayo Dar es salaam na Kilimanjaro,” alisema majambazi hao walikuwa wakitumia mbinu ya kupanga nyumba za kulala wageni na kubadilisha vyumba kila mara ili waweze kutekeleza azma yao.

Wakati huohuo, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema jambazi mmoja ambaye amekuwa akijihusisha na utekaji katika minada ameuawa baada ya mapambano na polisi.

Alisema wezake walitokomea kusikojulikana baada ya mapambano hayo katika kijiji cha Simbay wilayani Hanang’.

Alisema jambazi huyo aliyeuawa alijulikana kwa jina moja la Juma na kwamba anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35-40.

Alisema polisi walimfyatulia risasi ambazo zilimpata mguu wa kulia, mkono wa kulia na mgomgoni na akakosa nguvu na kukamatwa.

“Majambazi hawa inasemekana walikuwa wanaenda kufanya utekaji katika mnada wa Endasaki uliopo Katesh, lakini pia alikiri kuwa wamekuwa wanafanya hivyo katika minada mingine kwa kutumia silaha zilizounganishwa kienyeji,” alisema.

“Askari wangu walipofanya upekuzi wa vitu alivyokuwa nanyo walikuta silaha iliyotengenezwa kienyeji, panga mbili na katani zilizosokotwa zinazotumika kulipua fataki ambazo wamekuwa wanazitumia kwenye uhalifu.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page