top of page

RAZACK ABAROLA ATAJA SIRI YA PENALTI ZA URA

  • Khalidi
  • Jan 15, 2018
  • 1 min read

Mlinda mlango wa timu ya Azam, Razack Abarola, raia wa Ghana, amefunguka kuwa hali ya kujiamini na kuwa makini ndiyo iliyochangia kwake kuweza kuzidaka penati mbili za wapinzani wao URA ya Uganda katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Abarola aliisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa Mapinduzi baada ya kudaka penati mbili kati ya tano za timu ya URA katika fainali ya kombe hilo iliyopigwa juzi Jumamosi katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mghana huyo amesema kuwa tofauti ya makipa wengine ambao wanakuwa hawana umakini inapofika hatua hiyo, lakini kwake yeye aliongeza hali hiyo kwa kuamini hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kusaidia timu yake kuchukua ubingwa huo.

“Nilijipanga muda mrefu kuisaidia timu yangu katika hali yoyote ile, ndiyo maana hata nilipofika katika penalty wala sikuwa na hofu na ndiyo nikaongeza kujiamini kwa kuona hii ndiyo nafasi ya kuisaidia timu yangu kutwaa ubingwa na kweli ikawa hivyo.

“Ubingwa wetu huu tunautoa zawadi kwa mashabiki wetu ambao wamekuwa wakitusapoti katika kila hali na hata tulipokuja huku Zanzibar tulijua kwamba tuna deni kwao na kitu kimoja tuseme kwamba tutaenda kupigania makombe mengine ambayo tunashiriki kwa ajili ya kuyatwaa,” alisema Mghana huyo.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page