top of page

BEKI KISIKI SIMBA AREJEA…

  • Fahari News
  • Jan 15, 2018
  • 1 min read

Ukuta wa Simba kwa sasa unaendelea kuimarika baada ya Beki wao Kisiki, Salim Mbonde aliyekuwa majeruhi kuanza mazoezi ambapo kama mambo yatamuendea vinzuri anaweza kuwemo katika kikosi cha timu hiyo itakayochenza zidi ya Singida United.

Mbonde ambaye alitua Simba katika usajili wa dirisha kubwa akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, amekosekana katika kikosi hicho kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na kujiuguza jeraha la goti.

Mkuu wa kitengo cha habari cha Simba, Haji Manara, amesema wachezaji wetu waliokuwa na majeraha ya muda mrefu wameanza kupona kwa sasa, baada ya Shomary Kapombe kurejea, na kwa sasa Mbonde na Said Mohammed ‘Nduda’ nao wameanza mazoezi mepesi.

“Kwa sasa wanafanya mazoezi mepesi na baada ya muda watajumuika na wenzao, kama wakiwa fiti basi wanaweza kutumika katika mchenzo dhidi ya Singida United,” alisema Manara.

Mbonde alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili huku akiweka kibindoni kiasi cha milioni 30 kama ada yake ya usajili.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page