top of page

ASKOFU KAKOBE AELEZA ALIVYOHOJIWA NA TRA

  • Khalidi
  • Jan 15, 2018
  • 1 min read

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowshp (FGBF), Zachary Kakobe ameeleza namna alivyohojiwa na tume mbili zilizoundwa kwa nyakati tofauti na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na kutoa mrejesho wa kazi zilizofanywa na tume hizo.

Askofu Kakobe ametoa mrejesho huo wakati wa Ibada katika kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es salaam, ikiwa ni mara ya pili kuzungumzia sakata hilo akiwa na waumini wake tangu Desemba 31 mwaka jana.

Hata hivyo Kakobe alisema kutoa mrejesho huo hakuwazuii TRA kueleza waliyobaini, lakini amesema azungumze mapema na waumini wake kwa kuwa ndio watoa sadaka na wana haki kwa asilimia 100 kujua kinachoendelea kanisani kwao.

“waliuliza kuhusu utajiri wangu, niliwaambia ninanyumba moja tu duniani ipo kijitonyama niliijenga kwa gharama y ash 2 milioni na kiwanja nilinunua sh 30,000. Ninanyumba ya kawaida na ipo katika mtaa wa kawaida uitwao kwa Kakobe. Utafuteni mtaiona nyumba yangu.”

Askofu Kakobe alisema aliwaeleza wazi kuwa anawaumini wake ambao hawakuridhishwa na anapoishi, hivyo walitamani awe na sehemu nzuri itakayoweza kufaa kwa ajili ya wageni wa kimataifa wanaoweza kuwatembelea. Alisema walimshirikisha hilo na walijenga eneo jingine kwa michango yao miaka 10 iliyopita.

Alisema suala la akaunti za kanisa aliliweka wazi na kuwaambia kuwa kuna akaunti benki ya NBC na akaunti ya mfuko wa kitaifa wa FGBF iliyopo pia NBC Meru, Arusha.

“Niliwaambia wazi mimi wala mke wangu hatuna akaunti benki. Binafsi sina mradi wowote, sina shamba, sina kuku hata mmoja, paka na wala panya niliyefuga. Niliwaambia hata kanisa hatuna mradi wowote wa kiuchumi na hivi ndivyo tunavyoishi,” alisema.

留言


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page