top of page

AKAMATWA NA MAMILIONI UWANJA WA NDEGE DAR

  • Khalidi
  • Jan 15, 2018
  • 1 min read

Jeshi la polisi kitengo cha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), linamshikilia mfanyabiashara wa vifaa vya magari, Boniface Mbilinyi (32) kwa tuhuma za kusafirisha dola za Marekani 83,000 (Sh milioni 182.6).

Kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kumetokana na kuimarika kitengo cha ukaguzi uwanjani hapo kama sehemu ya udhibiti mianya ya kuifanya Tanzania kama sehemu ya kupitia au kutoa kitu chochote bila utaratibu.

Kamanda wa polisi Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha fedha hizo kwenda Dubai.

Alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa na polisi Januari 13 saa 9 alasiri uwanjani hapo kwa kushirikiana na maofisa wa Forodha na alikuwa akisafiri na dola za Marekani 123,000.

Alisema kati ya hizo, dola 40,000 za Marekani zilithibitishwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) LAKINI DOLA 83,000 ZA Marekani hakuzitolea taarifa yoyote.

“Tulimkamata akiwa anakaguliwa eneo la ukaguzi wa uwanja huo, Mtuhumiwa tunamshikilia kwa mahojiano hivyo tunategemea kesho kupeleka jalada kwa Mwanasheria wa serikali aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Mbushi.

تعليقات


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page