top of page

VITUO 1 2 VYA MAFUTA VYAFUNGWA NA TRA

  • Khalidi
  • Jan 14, 2018
  • 1 min read

Mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) imevifungia vituo 12 vya mafuta mkoani Kilimanjaro kutokana na kuendesha biashara bila ya kuwa na mashine za kutolea lisiti za kielektroniki

Vituo hivyo vinadaiwa kukiuka makubaliano ambayo wafanya biashara walitakiwa kuweka mashine maalumu ambazo zina uwezo wa kutoa stakabadhi za kielectroniki (EFD) kwa wateja wake ifikapo Desemba 31/2017

Meneja wa TRA mkoani Kilimanjaro Msafiri Mbindi alithibitisha kufungwa kwa vituo hivyo mkoani Kilimanjaro

Kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 na kanuni zake za mwaka 2016 mfanyabiashara anethibitishwa kukwepa kutumia au kutoa risiti za kielectroniki anaweza kukabiliwa na adhabu ya faini ya Sh milioni 3 hadi milioni 4.5

Aidha sheria hiyo imeeleza mnunuzzi anaekutwa na kosa la kutodai risiti adhabu yake ni faini kati ya Sh 30,000 hadi 150,000 au kifungo au adhabu zote kwa pamoja

Hata hivto TRA Kilimanjaro imebuni mbinu mpya ya kufanya kazi kwa kupiga kambi katika Baa kubwa na klabu za usiku ambazo ni maarufu, hatua ambayo inachukuliwa kuwakumbusha wafanya biashara kutoa risiti za EFD

留言


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page