top of page

MBEZI BEACH KINARA MIGOGORO YA ARDHI

  • Khalidi
  • Jan 11, 2018
  • 1 min read

Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amelitaja eneo la Mbezi Beach wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam kuongoza katika migogoro ya ardhi iliyosababishwa na wapigaji dili.

Akisikiliza kero za wananchi wa Dar es salaam Lukuvi alisema jitiada za makusudi zinatakiwa kuondoa migogoro hiyo ili kuleta amani nchini.

Alisema amechoshwa na utapeli uliokuwa ukifanyika katika Wilaya ya Kinondoni, hasa Mbenzi Beach, hivyo kwa sasa atahakikisha kero hiyo inakuwa historia.

Alisema tangu aanze kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wiki hii, tayari amesikiliza malalamiko zaidi ya 250 na Mbezi Beach imezidi kwa matatizo ya ardhi kuliko sehemu yoyote hapa nchini.

Lukuvi aliwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha kusikilizaa migogoro hiyo ili serikali iweze kutenda haki kwa kuwapata wamiliki halali.

Lukuvi alisema upimaji holela wa awali ulisababisha baada ya kuanza kupima ardhi ulionekana umegawa hati nyingi kuliko eneo lililopo.

Lukuvi amewaagiza maofisa ardhi kuwasaka kwa udi na uvumba wote wanaojihusisha na utapeli wa viwanja katika Mkoa wa Dar es salaam.

留言


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page