top of page

MAJALIWA AWATIA KIBARUANI MWIGULU,MBARAWA SWALA LA MBOLEA

  • Khalidi
  • Jan 11, 2018
  • 1 min read

Ikiwa imebaki siku moja kwa kwa waziri wa kilimo Charles Tizeba kutekeleza agizo la Rais Magufuli kusambaza mbolea nchini

Waziri Mkuu Kassim majaliwa amesema ameridhishwa na usafirishwaji wa mbolea kutoka kwa wasambazaji wa mbolea nchini kwenda kwa wakulima

Pia amemuagiza waziri Tizeba kushirikiana na waziri wamambo ya ndani ya nchi Mh Mwigulu Nchemba na waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliana prof Makame Mbarawa kuhakikisha mbolea inafika haraka kwa wakulima

Sambamba na hilo ameitaka kampuni ya usambazaji mbolea Nchini Tanzania (TPC) kuwa na mikakati madhubuti itakayowezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati wote nchini

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka katika ofisi ya waziri mkuu taarifa ilieleza kuwa waziri mkuu alisema serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuletea tija

Alieleza kuwa aliitaka (TPC) kuwa iwe inafanya maandalizi ya usambazaji wa mbolea mapema kwa sababu serikali inataka wakulima wapate pembejeo za kilimo miezi miwili kabla kuanza kwa msimu

Katika taarifa hiyo alieleza kuwa waziri Mkuu alimtaka Dk Tizeba ashirikiane na waziri wa Mambo ya ndani na Nchi Dk Nchemba ili kuhakikisha maroli yanayobeba mbolea yanafika mkoa husika kwa wakati husika

Dk Tizeba pia aliagizwa na waziri Mkuu awasiliane na waziri wa ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano Prf, Makame Mbarawa ili marori yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele

“si kwamba yaongeze uzito hapana bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza “ alisisitiza waziri Mkuu kutoka katika taarifa hiyo

Comentarios


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page