top of page

KENYA AIRWAYS YAZINDUA SAFARI ZA MOJA KWA MOJA HADI MAREKANI

  • David
  • Jan 11, 2018
  • 1 min read

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limezindua uuzaji wa tiketi za safari ya kwanza kabisa ya ndege zake za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani.

Shirika hilo linapanga kufanya safari yake ya kwanza mnamo 28 Oktoba, hatua itakayoifanya Kenya Airways kuwa shirika la kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na safari za moja kwa moja Marekani.

Ndege za shirika hilo litakuwa zinafasiri moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa JFK, New York kwa ushirikiano na shirika la Delta Airlines la Marekani.

Meneja Mkurugenzi wa Kenya Airways Sebastian Mikosz akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema safari hizo zitawafaa sana katika mpango wake wa ukuaji wa shirikia na kuvutia abiria kutoka kwa mashirika na kampuni mbalimbali pamoja na watalii wa hadhi kufika Kenya na Afrika.

Safari hiyo itachukua saa 15 kutoka New York hadi Nairobi na saa 14 kutoka Nairobi hadi New York na litatumia marubani wanne na wahudumu 12 wa ndege ambapo Safari yote itatumia tani 85 za mafuta huku shirika hilo likitumia ndege zake za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner ambazo huwabeba abiria 234.

Kwa mujibu wa Bodi ya Utalii Kenya, Kenya hupokea watalii 100,000 kutoka Marekani kila mwaka na safari hizo zinatarajiwa kuifanya nafuu kuzuru Kenya kwa kupunguza muda wa kusafiri na gharama.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page