top of page

ALIYEKIMBIA NA MASHINE YA EFD AKAMATWA

  • Khalidi
  • Jan 11, 2018
  • 1 min read

Mtendaji wa kata ya Nhundulu wilayani Misungwi, Paul Mayila amemtia mbaroni Mtendaji wa kijiji cha Mwawile katika kata hiyo (VEO), Felician Mhala aliyedaiwa kukimbia na mashine ya risiti ya electroniki (EFD) na kitabu cha kumbukumbu ya makusanyo ya ushuru wa mazao.

Mayila alimkamata VEO huyo baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Sweda kuagiza waliotafuna fedha za makusanyo ya mapato ya halmashauri wakamatwe ili kuhojiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na maadili.

Sweda alitoa agizo hilo baada ya kamati ya Fedha, Uongozi na mipango ya Halmashauri hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake,Anthony Bahebe kutembelea vyanzo vya mapato kubaini sababu zilizosababisha kushuka mapato ya halmashauri hiyo Novemba 2017 kutoka sh milioni 170 hadi sh milioni 88.

Bahebe alisema VEO alikamatwa na ofiasa mtendaji wake wa kata aliyempeleka katika Halmashauri hiyo ili kuwasilisha nyaraka na fedha za makusanyo ya lango la Mwawile.

“Mtendaji wa Kijiji cha Mwawile aliyetukimbia na kitabu na mashine ya kutolea risiti tulipokuwa na wajumbe wa kamati ya wataalam tuliongozana nao.

Januari 4 mwaka huu baada ya Mhala kukimbia, Diwani wa Kata hiyo, Faustine Msafiri alisema kuna mgogoro katika lango hilo ndiyo maana mashine ya EFD na kitabu hicho viliondolewa wasibaini madudu yaliyopo.

コメント


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page