top of page

WINNIE MANDELA KATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA UGANDA

  • Fahari News
  • Jan 9, 2018
  • 1 min read

Aliyekuwa mke wa Nelson Mandela, Rais wa kwanza mzalendo Afrika kusini, Winnie Madikizela-Mandela, anatarajiwa kutunikiwa shahada ya heshima na Chuo Kikuu kikongwe Afrika Mashariki, Makerere , wakati wa mahafari yake ya 68 baadaye mwenzi huu yatakayofanyika kwa siku nne mfululizo.

Mahafali hayo yatafanyika kuanzia Januari 16 na kuendelea hadi Januari 19, mwaka huu huku idadi ya wahitimu ikiwa 15,172.

Winnie, mwanasiasa na mwanaharakati wa Afrika kusini mwenye umri wa miaka 81, atatunukiwa Shahada ya Heshima ya sheria ili kutoa mchango mkubwa alioutoa katika kupigania uhuru dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini mwake.

Mama huyu ambaye kitaaluma ni muuguzi, alikuwa bega kwa bega na mumewe aliyewachachafya makaburu, kiasi cha kumtafutia sababu kadhaa na hatimaye kumtupa jela mwaka 1964.

Mandela alikua ni mwanasheria kitaaluma alitumikia kifungo kwa miaka 27, lakini alipoachiwa aliibuka shujaa na kuchaguliwa kuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini. Alistaafu Urais mwaka 1999 na alifariki dunia Desemba 5, mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95.

Taarifa kutoka ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Makerere imesema katika mahafali ya mwaka huu, wanafunzi 11,300 watakuwa na shahada ya kwanza na diploma, 436 ni wa shahada za uzamili wakati 36 watatunukiwa shahada za Udaktari wa Falsafa (PhD).

Kommentare


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page