top of page

MFUNGWA AKAMATWA MTAANI NA BUNDUKI

  • Khalidi
  • Jan 9, 2018
  • 1 min read

Katika taarifa ya jeshi la polisi mkoani Mara kutoka kwa Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed ilieleza kuwa mfungwa Musa Bheha na wenzake watatu walikamatwa saa 12:00 jioni ya Januari 3 katika Kijiji cha Robanda baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Musa Bheha, ambaye ni mkazi wa Rufiji mkoani Pwani, alitakiwa kuwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kutiwa hatiani katika shauri la uhujumu uchumi namba 5/2015. Lakini amekamatwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa), akituhumiwa kujihusisha na ujangili Kamanda Mohamed alisema watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na meno manne ya tembo yenye uzito wa kilo 72.4, bunduki mbili – moja ya kivita aina ya AK-47 na Rifle pamoja na risasi 130. “Walikuwa na bunduki aina ya Riffle 458 na risasi tano zimefichwa katika uzio wa nyumba na baada ya mahojiano walikiri kuua tembo wawili ndani ya Hifadhi ya Serengeti Januari 2,” alisema. Alisema baada ya kubanwa zaidi mmoja wa watuhumiwa hao aliwapeleka askari eneo walikokuwa wameficha bunduki aina ya AK-47. Akimzungumzia mfungwa huyo, Kamanda Mohamed alisema mtuhumiwa huyo ni mfungwa aliyepaswa kuwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu MkaziWilaya ya Musoma mwaka jana. Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa wiki tatu baada ya kuhukumiwa, kuliibuka taarifa kuwa alipewa adhabu ya kifungo cha nje cha kutumikia jamii jijini Dar es Salaam ambako hata hivyo imebainika hajawahi kufika, suala ambalo pia polisi wamelianzishia uchunguzi

Ni kawaida kukutana na wafungwa mitaani wakiwa wanasimamiwa na askari Magereza, lakini si kwa Kassim Musa Bheha

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page