top of page

MAWAZIRI WALIOACHWA KUENDELEA NA KAZI

  • Fahari News
  • Jan 9, 2018
  • 1 min read

Ikulu ya Kenya imetangaza kuwa mawaziri wote wataendelea na kazi hadi wateule wapya wachunguzwe, wathibitishwe na kuapishwa.

Ijumaa iliyopita Rais Uhuru Kenyatta alitangaza baraza la mawaziri linalojumuisha watu sita waliokuwepo kwenye serikali ya awamu ya kwanza ya utawala wake na watatu wapya. Msemaji wa Ikulu ya Kenya, Manoah Esipisu amesema, mawaziri wote wa zamani wameagizwa kuendelea kutekeleza wajibu wao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Esipisu, tangazo la Mkuu wa Utumishi wa Umma la Desemba mwaka jana limeagiza viongozi hao waendelee na kazi hadi watakaposhauriwa vinginevyo.

Wakati wowote kuazia sasa Kenyatta atatangaza mawaziri wengine kujaza nafasi 13. Esipisu amesema, Rais atateua mawaziri kwa kuzingatia sifa ya mhusika, ‘usafi’, uchapakazi katika utumishi na vifungu vya Katiba ya nchi.

Mawaziri waliokuwa katika Serikali iliyomaliza muda wake na sasa wameteuliwa tena ni aliyekuwa Waziri wa Elimu, DK Fred Matiang’i.

Matiang’i ameteuliwa tena kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Kaimu Waziri wa Elimu, Wengine ni Henry Rotich (Fedha), Najib Balala (Utalii), James Macharia (Usafirishaji), Joe Mucheru (ICT) na Charles Keter (Nishati).

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page