WAWILI WAHOFIWA KUFA KWENYE MGODI BAADA YA KUFUNIKWA KWA SIKU 7
- Khalidi
- Jan 8, 2018
- 1 min read

Wachimbaji wawili wadogo wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Sekenke moja, Iramba wanahofiwa kufariki dunia ,baada ya kuzama katika maji na kufukiwa na kifusi cha udongo wakiwa ndani kwa siku saba. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iramba, Bwana Emmanuel Luhahula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema awali wachimbaji hao waliofukiwa walikuwa watano lakini watatu walifanikiwa kuokolewa huku wengine wawili wakikwama kwenye mgodi huo wenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita 150. Aidha Luhahula amesema kuwa bado wanaendelea na kazi ya kutafuta miili ya watu hao hivyo amesimamisha shughuli za uchimbaji na kutoa siku mbili za utafutaji na kama itashindikana atafunga mgodi huo. Wachimbaji hao wa madini watano inadaiwa walifukiwa na kifusi hicho Disemba 31, 2017
Comments