top of page

CHADEMA WAFUNGA MDOMO HOSPITALI ALIYOLAZWA LISSU

  • Khalidi
  • Jan 8, 2018
  • 1 min read

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu amewasili salama Ubelgiji alikokwenda kwa ajili ya matibabu huku chama chake na familia yake wakificha jina la hospitali aliyofikia nchini humo

Kwamujibu wa mtandao wa http://hospitals.webometrics.info/en/europe/belgium%20 unasema kuwa Hospitali kali tano ambazo moja wapo huenda mbunge huyo atakua maefikia ni univesitair Zienkenhuis (UZ Leuven) inayoshika nafasi ya 63 kwa ubora duuniani, Hospitali ya Bruxellles Cliniques Universitaires saint Luc ( ya 545 duniani) Universitair brugmann Antwerpen (700) Centre Hospitalier Universitaire de Brugmann (941) na HÔpital universitaire des Enfants Reine Fabiola (991)

Mbunge huyo alisafirishwa kwa ndege ya KLM iliyomchukua kutoka Amstedam, Uholanzai, aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zaventem juzi saa 11: 40 jioni na kupokelewa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi

Rais huyo wa chama cha wanasheria (TLS) alianza safari yake ya tatu ya matibabu akitokea nchini Kenya, Nairobi kwa ndege ya KQ

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mboye alisema hospitali anayotibiwa mbunge huyo nchini humo kwa sasa ni siri kwa sababu za kiusalama

Mboye ambae pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni alisema “Jua kwamba yupo nchini Ubelgiji , baadae itajulikana baada ya kuhakikisha kuwa utaratibu wote wa kiusalama upo vizuri”

Kauli ya Mboye iliungwa mkono na mdogo wake Lissu Vincent Mghwai ambae alisema “kwa ababu za kiusalama sio lazima kujua Hospitali, itoshe kufahamu kuwa yupo Ubelgiji, amefika salama amepokelewa vizuri na kila kitu kinaenda vizuri sana" alieleza zaidi Mgwai

Lissu alishambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasio julikana September 7 wakati akijandaa kushuka kutoka kwenye gari lake nyumbani kwake Area D mjini Dodoma alipokuwa akitokea Bungeni.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page