top of page

BENKI KUU YASHUSHA RUNGU KWA BENKI TANO

  • David
  • Jan 4, 2018
  • 1 min read

Ikiwa ni wiki chache baada ya Rais Magufuli kusema Benki zisizofanya vizuri zigungwe, Leo Benki Kuu imeziweka Chini ya usimamizi wa Bodi ya Bima ya Amana Benki tano kufuatia kusuasua katika uendeshaji wake na udogo wa mitaji.

Benki Kuu imechukua hatua hii ili kulinda amana za wateja katika Benki hizo na kuepusha kuyumbisha mfumo wa Benki nchini.

Benki zilizowekwa kwenye uangalizi wa Bodi ya Bima za Amana ni Efatha, Covenant Bank, Njombe Community Bank, Kagera Farmers Cooperative Bank and Njombe Community Bank.

Hii sio Mara ya kwanza Benki Kuu kuchukua hatua kama hii. Kwa siku za karibuni Twiga Bankcorp na FBME nazo zilikumbwa na uamuzi kama huu.

Sekta ya Kibenki Nchini Tanzania yenye mabenki zaidi ya 50 ni moja ya muhimili muhimu kwa ustawi wa Uchumi.

Kommentare


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page