top of page

NYOKA WAKUBWA 50, PIMBI 300 WAHAMISHWA IKULU CHAMWINO

  • Fahari News
  • Dec 22, 2017
  • 1 min read

Zaidi ya wanyamapori 400 wamehamishwa kutoka katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma na kupelekwa katika pori la Akiba la Swagaswaga lililopo kilometa 130 kutoka mjini humo,

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), DK. James Wakibara alisema hayo

Alielezea kuwa wanyamapori hao, waliokuwa Ikuli ya Chamwino na ambao wamepelekwa kwenye pori la Swagaswaga ni pimbi 300, nyoka wakubwa 50, kenge, na mijusi kadhaa.

“Tumefanikiwa kuwahamisha wanyama hao kwa usalama, kitendo kinachodhihilisha kuwa wataalamu wetu wa TAWA wamebobea katika fani hii ya wanyamapori,” alifafanua DK Wakibara.

Mkurugenzi huyu alisema kuwepo kwa wanyama hao Ikulu ya Chamwino , kumesaidia kuongeza thamani ya pori hilo jipya la Akiba, ambalo kwa sasa linaandaliwa kuwa eneo la utalii kwa wakazi wa miji ya Dodoma, Singida na Babati mkoani Manyara.

Kaimu mkurugenzi wa raslimali za wanyamapori, David Kanyata alisema TAWA bado inawafuatilia kwa karibu wanyamapori hao waliohamishwa pori la Swagaswaga kutoka Ikulu ya Chamwino.

“Wanaendelea vinzuri , mazingira ya poli hili la Akiba ni sawa nay ale ya Dodoma, maana pori hili pia ni eneo lililosheheni nyoka wakubwa wa kila aina, tembo, Simba, Chui, Nyati, Pimbi, Swala, Mijusi na kila aina ya ndege,” alisema.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page