MWANAMKE AJIFUNGUA WATOTO WANNE
- Fahari Neews
- Dec 22, 2017
- 1 min read

Mwanamke mmoja Asha Mashaka(27), amejifungua watoto wanne kwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Morogoro huku akiomba msaada kwa serikali na wasamalia wema kumsaidia malezi.
Tukio hilo kwanza mama huyo kwa kujifungua idadi hiyo ya watoto katika hospitalini hapo, ambapo mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (CCM) alifika Hospitalini hapo kumjulia hali na kutoa msaada kwa mzazi huyo.
Asha alisema awali alifahamu kuwa ana mapacha tu baada ya kupimwa kipimo cha Ultra-sound na kufanyiwa upasuaji alipata watoto wanne wawili wa kiume na wawili wa kike.
Alisema katika familia yake nay a mumewe wana historia ya kuzaa watoto mapacha hivyo katika maisha yake aliamini upo uwezekano wa kuzaa watoto mapacha japo kuwa hakufikilia kama atazaa watoto wanne.
“Huu ni uzazi wangu wa pili, mimi mwenyewe ni pacha na hata kwenye familia ya mume wangu pia kuna mapacha, nashukuru mungu kwa zawadi hii namuomba mungu anikuzie na sasa ninajumla ya watoto watano,” alisema Asha.
Aidha aliomba serikali na wadau mbalimbali kumsaidia malezi ya watoto hao hasa katika kipindi hiki cha uchanga ambapo kuna mahitaji mengi ya watoto kwani mume wake ni mkulima wa bustani za mbogamboga nay eye mwenyewe ni mama wa nyumbani.
Alitaja baadhi ya mahitaji yanayotakiwa kwa sasa kwa watoto hao kuwa ni pamoja na maziwa, nguo za watoto, blanketi, pampas, sabuni na mahitaji mengine yanayowahusu watoto wachanga.
Ofisa muuguzi msaidizi wa wodi ya watoto wachanga wenye uzito mdogo, Nasra Bakari, alisema hali ya mama huyo inaendelea vinzuri ingawa si msemaji wa hospitali
Comments