top of page

LONDA APONEA CHUPUCHUPU, MOGELLA AKALIWA KOONI NA YONO

  • Khalidi
  • Dec 22, 2017
  • 1 min read

Operesheni ya wadaiwa sugu wa Kiwanda cha Urafiki, imewakumba wapangaji zaidi ya 160 kuondolewa huku Meya wa zamani wa Halmashauri ya Kinondoni, Salum akiponea chupuchupu.

Miongoni mwa wapangaji wa urafiki Kota waliokumbwa na kadhia hiyo ni ni mchezaji wa zamani wa Yanga, Zamoyoni Mogella.

Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Shadrack Nkelebe alisema wanawadai wapangaji wao kati y ash 600 milioni hadi sh 1 bilioni huku Londa aliyekuwa akidaiwa sh 18.7 milioni akilipa.

“Hkuna msalia mtume katika hili, tutawatoa wote bila kujali nani ni nani. Tumeshaaza kuwatoa na wengine tumepata notisi,” alisema Nkelebe “kila anayedaiwa anapaswa kulipa, haiwezekani kutoka mwaka 2015 mtu halipi na hawa ambao wamevamia tutawatoa.”

Nyumbani kwa Londa aliyepanga nyumba ya kiwanda hicho iliyopo mtaa wa Ngano, Kata Hananasif wilayani Kinondoni alikuwa akihaha kulipa deni hilo huku familia yake ikijitosa kuokoa vitu visibebwe na Yono uongozi wa kiwanda na Yono mara baada ya kufika nyumbani kwake saa 7:55 mchana

kumuondoa ikiwa teyari wameanza kuvunja makufuri, Londa alipiga simu kuzuia ili apewe muda kufikia saa 9:30 alasiri awe amelipa deni lililokubaliwa na yeye kulitimiza kwa kulipa sh 18.7 milioni.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page