BIASHARA ZADODA KARIAKOO
- Fahari News
- Dec 22, 2017
- 1 min read

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la kariakoo, Dar es salaam wamelalamikia uhaba wa wateja wa bidhaa zao katika musimu huu wa sikukuu za krisimasi na mwaka mpya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wafanyabiashara hao wamesema hali ya biashara katika sikukuu hizi ni tofauti ba nyingine zilizotangulia.
Mmoja wa wafanyabiashara wa nyanya katika soko hilo, Jenifa John, alisema soko hilo, kwa sasa halina wateja wa kutosha jambo ambalo linazifanya bidhaa zao kuharibika.
“Kama unavyoona mwandishi kweupe, ukiangalia unaona hadi mwisho wa soko wakati sikukuu nyingine siku kama hizi za mwisho wateja wangekuwa wengi sana,” alisema Jenifa.
Comments