top of page

KIBANO CHAIVA KWA VIGOGO ‘DILI’ AIRTEL

  • Khalidi
  • Dec 21, 2017
  • 1 min read

Hatimaye siku zimeanza kuhesabika kubaini ukweli wa kila kitu kilichotokea katika ‘dili’ la ubia linaloelezewa kuwa na utata ndani yake baina ya Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) na ile ya simu za mkononi Airtel.

Hiyo haitoshi, inaelezwa kuwa wote waliohusika katika kufanikisha ‘dili’ hilo, wakiwamo vigogo mbalimbali, huenda wasibaki salama dhidi ya kibano cha uchunguzi huo wa vyombo vya serikali katika kubaini ukweli na mwisho hatua stahiki kuchukuliwa.

Dalili za kawaida kwa kibano juu ya kila kilichofanyika katika ubia huo ambao hadi sasa unaipa TTCL umiliki wa asilimia 40 ya hisa, zilijidhihilisha jana mjini Dodoma wakati Rais Magufuli alipofichua kuwapo kwa ‘mchezo mchafu,’ hivyo mwishowe kuamuru uchunguzi kufanywa.

Waziri wa fedha na mipango DK. Philip Mpango, ndiye aliyepewa agizo la kufuatilia undani wa ‘dili’ hilo la TTCL NA Airtel kutokana na kile alichoeleza Rais Magufuli kuwa ni kuwapo kwa taarifa kwamba Airtel ni mali ya TTCL.

“Agizo hilo la Rais linamaanisha kwamba hakuna kitakachojificha… kama kuna yeyote alikiuka sheria za nchi kwa sababu yoyote ile atakumbana na kibano cha mkondo wa sheria kwasababu serikali hii haina masihara linapokuja suala la kupigania maslahi ya Taifa.”

Akiwa mjini Dodoma jana, Rais Magufuli alitoa agizo la kuchunguzwa kwa suala hilo la TTCL, na Airtel kwa DK. Mpango alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jingo la ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Comentarios


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page