top of page

AJALI YA BASI YAUA SABA KIGOMA

  • Khalidi
  • Dec 21, 2017
  • 1 min read

Watu saba wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Hiace katika kijiji cha Kabeba Tarafa ya Ilagara mkoani hapa.

Ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Scania mali ya Kampuni ya Saratoga lenye namba za usajili T 384 BMG lililokuwa linatoka katika kijiji cha Rukoma kwenda Kigoma Mjini na hiace yenye namba za usajili T 237 BCE iliyokuwa ikitokea Kigoma Mjini.

Akizungumza kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike, alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Bosco na dereva wa Hiace alifahamika kama Hassan.

Alisema majina ya marehemu na majeruhi bado hayajafahamika na kwamba majeruhi wote wamepelekwa kituo cha Afya ILGL kwa matibabu.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page