top of page

DK MPANGO AALIKA WAWEKEZAJI

  • Khalidi
  • Dec 20, 2017
  • 2 min read

Waziri wa fedha na mipango, DK. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Balonzi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad na kutoa wito kwa wawekezaji kutoka nchi hiyo kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali, zikiwamo nishati, misitu, kilimo, gesi na mafuta.

DK. Mpango amemueleza Balozi huyo kwamba Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda na kwamba wawekezaji kutoka Norway watakuwa na mchango mkubwa wa kuwezesha kufikiwa lengo hilo. Aliyataja maeneo ya kuongeza thamani ya mazao ya misitu,

mifugo,uvuvi, nishati, kilimo na mengine mengi kwamba yataongeza tija katika sekta hiyo na kwamba malighafi za kilimo zitachochea uzalishaji katika viwanda na kuinua kupato cha wananchi.

“Tumeamua kujenga Reli ya kati kwa viwango vya kimataifa-SGR, ambayo inahitaji umeme wa kutosha,kwahiyo bado tunahitaji mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Norway ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na nishati ya umeme ya kutosha nay a uhakika ili kufanikisha mradi huo mkubwa,” alisema DK. Mpango.

Kuhusu sekta binafsi DK. Mpango alisema kuwa serikali Serikali imeendelea na majadiliano na sekta hiyo ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili, ikiwamo masuala ya kodi na kujenga kuaminiana kati ya pande hizo mbili.

Alifafanua kuwa sekta binafsi ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa taifa na kwamba vikao vya mara kwa mara vimeanza kuzaa matunda.

Kwa upande wake Balozi Kaarstad, alisema nchi yake imelidhika na namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya watu wake kupitia kuhamasisha uchumi wa viwanda.

Alisema nchi yake imesaini mikataba mikubwa miwili hivi karibuni, ikiwamo wa msaada wa krona milioni 600 (fedha za Norway) kwa mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA, hatua inayoamini kuwa itaharakisha maendeleo na uchumi wa kati wan chi ifikapo mwaka 2025.

Comentarios


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page