top of page

BABA ADAIWA KUWABAKA WANAWE WANNE TABORA

  • Khalidi
  • Dec 20, 2017
  • 1 min read

Mkazi wa kijiji cha Chagana, Kata ya Lugubu, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Masanja Musoma (47), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake wanne wa kike.

Mwendesha mashtaka Msaidizi wa polisi, Alex Kataya, alidai mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, kuwa kati ya Novemba na Desemba 2017 katika kijiji cha Chagani, Kata ya Lugubu, mshtakiwa aliwabaka watoto wake wanne kwa siku tofauti.

Kataya alidai kuwa baada ya mtuhuiwa kuendelea kufanya vitendo hivyo, taarifa ziliwafikia polisi na kufanikiwa kumkamata Desemba 6, mwaka huu.

Alidai kuwa mtoto wa kwanza ana miaka minane, wa pili miaka kumi na wa tatu ana miaka 12 na wan ne anamiaka 13.

Aliendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 158 cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, inayozuia kutenda makosa hayo.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na mwendesha mashtaka aliwasilisha mahakamani hati ya kiapo akiomba mahakama kutompatia dhamana kwa kile alichodai anaweza kuharibu ushahidi wa kesi hiyo.

Hakimu Milanzi aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 20 (leo) itakapotajwa tena na mshtakiwa alipelekwa mahabusu.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page