NAMBA 8 NA 24 ZA KOBE ZASTAAFISHWA LAKERS
- Admin
- Dec 19, 2017
- 1 min read

Kobe Bryant amekuwa mchezaji wa kwanza wa NBA katika historia kuwa na jezi 2 zilizostaafishwa na timu moja, ambapo tukio hilo limefanyika leo, jezi zake namba 8 na 24 zimenyanyuliwa katika dimba la Staple Center na kustaafishwa.
Gwiji huyo wa Lakers amepewa heshima hiyo katika kipindi cha mapumziko kwenye mechi asubuhi ya leo kati ya Lakers na mabingwa watetezi Golden State Warriors.
Msemaji wa Lakers juzi alithibitisha timu hiyo kuwa na mpango wa kustaafisha jezi zote,namba 8 na namba 24, akielezea kuwa haiwezekani kustaafisha namba moja na kuiacha nyingine kwani alipata mafanikio katika namba hizo zote
Kobe ametumia misimu yake yote 20 ya NBA akiwa na Lakers, akishinda mataji katika jezi hizo 2.
Alicheza misimu 10 ya kwanza akiwa na jezi namba 8, akishinda ubingwa mara 3 mfululizo akiwa na mchezaji mwenzake Shaquille O'Neal, 2000-2002.
Mwaka 2006 akabadili namba na kuanza kuvaa namba 24, akiwa na jezi hiyo alishinda tuzo ya MVP 2008 na akaongeza makombe mawili ya NBA, 2009 & 2010.
Kobe mwenye umri wa miaka 39, amestaafu kucheza mpira wa kikapu mwaka 2016 akiwa na jumla ya makombe matano ya NBA
Comments