top of page

MAJERUHI WA AJALI WAHITAJI CT SCAN

  • Khalidi
  • Dec 19, 2017
  • 1 min read

Baadhi ya majeruhi wa ajali iliyoua watu watano na kujeruhiwa 14 Jumamosi katika Mtaa wa Buhongwa hapa jijini Mwanza wanahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa kutumia mashine ya CT Scan kufuatia hali zao kuwa mbaya, imeelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, DK Abel Makubi alisema baadhi ya majeruhi miongoni mwa 14 waliopokelewa wanahitaji uchunguzi wa kina ikiwemo kipimo cha CT Scan.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watano. Ajali hiyo ilihusisha gari namba T 107 BKK Toyota Coaster mali ya kampuni ya Auki wa Mwanza na lori aina ya Scania lenye namba T880ASA.

Kamanda Msangi alisema marehemu watano na majeruhi 13 wote ni abiria wa Toyota Coaster na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi dogo hilo.

Alisema dereva huyo alijaribu kupita magari mengine ya mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Alisema madereva wote wa magari hayo walikamatwa na kwamba watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi ukikamilika.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page