LEMA, NASSARI WALIA NA TAKUKURU
- Khalidi
- Dec 19, 2017
- 1 min read

Siku moja baada ya Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru) kusema kwamba haiwezi kuendelea na ushahidi uliotolewa na wabunge wawili wa Chadema,Joshua Nassari(Arumeru Mashariki) na Godbles Lema (Arusha Mjini), hatimaye wabunge hao wameibuka na kuishangaa.
Lema alisema hatua ya Takukuru kutupa ushahidi huo kutokana na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexandar Mnyeti aliyekuwa akituhumiwa kuhusika na kitendo cha kununua madiwani, kupandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Mkoa jambo lililofanya taasisi hiyo kumwogopa.
“Kwanzaa ninasikitika sana leo tunachombo cha kupambana na rushwa ambacho kimepelekea ushahidi wa kielektroniki wakapuuza, wakatupilia mbali ushahidi wa msingi.
“Haya majibu yamekuwa mepesi kwasababu aliyekuwa anatuhumiwa amepandishwa cheo na Rais, amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, maana yake Mkurugenzi wa Takukuru akichukua hatua dhidi ya Mnyeti, anakwenda kinyume na mteule,” alisema.
Hatua hiyo ya lema imekuja baada ya Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba akinukuliwa akisema kuwa wametupa ushahidi huo kutokana na kuingizwa siasa kwenye masuala ya uchaguzi. Kutokana na hali hiyo, Lema alisema taifa linahitaji Takukuru ambayo mkurugenzi anaweza akasimamia ukweli na pindi anapoona amepindishwa, aachie ofisi na kurudi nyumbani.
Bình luận