top of page

WAZIRI ATOA AJIRA KWA VIJANA

  • Khalidi
  • Dec 18, 2017
  • 1 min read

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwajage ameagiza Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kupitia upya mikataba ya kuifanyia kazi ili iweze kuimarisha utendaji wao.

Kadhalika, Mwijage ameagiza bodi hiyo kuunda mabaraza ya wafanyakazi ikiwamo kuwashirikisha wafanyakazi hao hadi kufikia februari 2018 iwe imeshaunda mabaraza hayo.

Waziri alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizindua bodi mpya y

a wakurugenzi wa TFC.

“Mikataba ya makubaliano yote yaliyofanywa na bodi iliyomaliza muda wake, tutaipitia upya kwa lengo la kuifanyia kazi..pia lazima kila kinachopitishwa kipate Baraka na bodi hii,” alisema waziri Mwijage.

Waziri Mwijage alisema serikali ni sikivu na kwamba haikubali mtu mwingine kupata faida kwa kutumia jina la TFC.

“Kwakuwahakikishia utendaji bora kutakuwa na timu ya kutosha; tutahakikisha mtoto wa baba anakula nundu,” alisema mwijage na kufafanua.

“Wapo wanaotaka kufanya biashara na sisi, lazima tupate faida kubwa na si bora faida. Hizi ni zam a za uzarishaji kwa tija kwa kutumia mbolea yetu.

Akifafanua zaidi, Mwijage alisema anaikabidhi kampuni hiyo kwa bodi na kwamba serikali itatoa kipaumbele katika biashara.

Waziri alisema pamoja na kwamba serikali itaipa kampuni hiyo kipaumbele katika ununuzi wa mbolea, lakini isibweteke.

“TFC isibweteke ikibebwa ibebeke…. Mkibweteka mbeleko itakatika.

Aidha , Mwijage alielezea ubora wa kampuni hiyo akisema wataalamu wamebaini kwamba ili mkulima aweze kutumia mbolea lazima ipimwe kwa kuwa udongo wa Temeke unatofautiana na ule wa Kinodnoni.”

Naye mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Profesa Egid Mubofu alisema anaahidi kupitia mikataba na makubaliano ili waweze kujiridhisha na kuhakikisha Tanzania inapata faida.

“Mheshimiwa waziri nakuahidi tutaunda mabaraza ili kusaidia utendaji wa bodi na kwamba bodi itapatikana wakati wote kwaajili ya kuimarisha ubora wa kazi,” alisema Prof Mubofu

Comentarios


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page