top of page

WATANO WAFARIKI KWA AJALI, 13 WAJERUHIWA

  • Khalidi
  • Dec 18, 2017
  • 1 min read

Watu watano wamefariki dunia na wengine 13 wamejeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T107 BBK Toyota Coaster mali ya Kampuni ya Auki ya jijini Mwanza, Kugongana uso kwa uso na gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 880 ASA.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ajali hiyo. Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema tukio hilo lilitokea katika Barabara ya Mwanza-Shinyanga, Kata ya Buhongwa jijini hapa. Alisema Coster iliyokuwa ikitokea Katoro mkoani Geita kuja jijini Mwanza, ilikuwa ikiendeshwa na Badru Habibu (33), mkazi wa Nyegezi na Scania hilo lilikuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea Dar es salaam. Kamanda msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa coster iliyokuwa imebeba abiria. Alisema kuwa dereva wa basi hilo dogo, alikuwa akiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari, ndipo aligongana na scania hilo.

“Nawaomba wananchi wafike katika hospitali ya Kanda ya Bugando ili kuitambua miili ya marehemu, maana tumehifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo. Pia majeruhi wote wapo hapo hapo hospitalini wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri,” alisema. Kamanda msangi alitoa wito kwa waendeshaji wa vyombo vya moto, hususani magari ya abiria, ya abiria, kuwa makini wawapo barabarani na kuendesha huku wakifuata kanuni, taratibu na sheria za barabarani.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page