top of page

POLISI WAWILI WATIWA MBARONI TAKUKURU

  • Khalidi
  • Dec 18, 2017
  • 2 min read

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imesema inachunguza watendaji wanne wa serikali wakiwamo askari polisi wawili kwa tuhuma za rushwa.

Wanaochunguzwa na taasisi hiyo nyeti ni wanasheria wawili wa baraza la uhifadhi wa Mazingira (Nemc), Bernard Kongole na Lucy Lwigisha na askari wawili wa kituo cha polisi Mbweni, Kinondoni jijini Dar es salaam, wote wakituhumiwa kwa rushwa ya Tsh. Milioni moja.

Wanne hao wanadaiwa kuomba rushwa hiyo kwa mkalimani ambaye anafanya kazi kwenye kiwanda cha uzalishaji mifuko ya sandarusi cha Yong Long Plastic Co. Limited kilichopo tegeta IPTL jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Thed Mjangira, alithibitisha taasisi hiyo kuwashikilia watu hao huku akibainisha kuwa upelelzi kuhusu suala hilo unaendelea.

“Nikweli tuliwaita kwaaajili ya kufanya nao mahojiano baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watu hao waliomba na kushawishi wapewe rushwa,” Mjangira alisema.

“Na naomba tu kwa sasa niseme hivyo kwa sababu upelelezi hauwezi kukamilika siku moja, tusubili mpaka utakapokamilika kwasababu bado tunaendelea kulifanyia uchunguzi zaidi.” Mjangira alimalizia kwa kusema hayo .Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imesema inachunguza

watendaji wanne wa serikali wakiwamo askari polisi wawili kwa tuhuma za rushwa.Wanaochunguzwa na taasisi hiyo nyeti ni wanasheria wawili wa baraza la uhifadhi wa Mazingira (Nemc), Bernard Kongole na Lucy Lwigisha na askari wawili wa kituo cha polisi Mbweni, Kinondoni jijini Dar es salaam, wote

wakituhumiwa kwa rushwa ya Tsh. Milioni moja.Wanne hao wanadaiwa kuomba rushwa hiyo kwa mkalimani ambaye anafanya kazi kwenye kiwanda cha uzalishaji mifuko ya sandarusi cha Yong Long Plastic Co. Limited kilichopo tegeta IPTL jijini Dar es salaam.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni,

Thed Mjangira, alithibitisha taasisi hiyo kuwashikilia watu hao huku akibainisha kuwa upelelzi kuhusu suala hilo unaendelea.“Nikweli tuliwaita kwaaajili ya kufanya nao mahojiano baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watu hao waliomba na kushawishi wapewe rushwa,” Mjangira

alisema.“Na naomba tu kwa sasa niseme hivyo kwa sababu upelelezi hauwezi kukamilika siku moja, tusubili mpaka utakapokamilika kwasababu bado tunaendelea kulifanyia uchunguzi zaidi.” Mjangira alimalizia kwa kusema hayo .

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page