top of page

MAKAMU WA RAIS ASEMA MIAKA SABA YA URAIS NI HOJA NZURI

  • david
  • Dec 16, 2017
  • 1 min read

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd amesema ushauri wa wajumbe wa Baraza la wawakilishi kutaka kuongezwa muda wa urais kutoka miaka mitano hadi miaka saba.

Balozi Iddi alizungumza hayo kwenye Baraza la wawakilishi wakati akifunga Baraza la tisa la wawakikishi lililodumu kwa wiki moja.

Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo Hamza Hassan Juma alisema ili kumpa Rais muda wa kutosha kutumikia wananchi ni vizuri muda wa urais ukaongezwa kuwa miaka saba.

Alisema pia kuongezwa kwa muda kutapunguza gharama za uchaguzi kutokana na uchaguzi kufanyika kipindi kifupi.

Akijibu ombi hilo Balozi Iddi alisema ni jambo lenye kuhusisha pande mbili za Muungano hivyo ni vizuri likaachiwa viongozi wa pande mbili kulifanyia kazi na kama litapita ni kweli linaweza kushusha gharama za uchaguzi.

Opmerkingen


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page