YANGA YAKUBALI MABADILIKO, MCHAKATO WAANZA JANGWANI
- Rehema Lucas
- Dec 15, 2017
- 1 min read

Klabu ya Yanga imetangaza kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko kwaajili ya maendeleo ya soka,ambapo watani wake wa Jadi Simba tayari tangaza kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kwamba Desemba 13 kulikuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho kilijadili ajenda mbalimbali.
Moja ya ajenda hizo ni kamati hiyo kuamua klabu iingie kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa kuruhusu kuingiza mwekezaji kwa ajili ya kuendesha klabu.
Mkwasa amesema kulingana na Katiba yao ya mwaka 2010, Ibara 56 kipengele cha 3 kinajieleza kuwa wanachama wanatakiwa kumiliki hisa 51 na 49 inaenda kwa mwekezaji.
“Kikao hicho halali cha Kamati ya Utendaji kiliridhia na kupitia klabu kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko kwani kwa sasa ni lazima kuendesha klabu kwa mfumo unaokwenda na wakati,” alisema Mkwassa.
Aliongeza kuwa, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga atatangaza mchakato mzima wa kuanza kwa mfumo huo na uongozi wa Yanga utafanya tathmini ya (Assert) za klabu ili kujua zina thamani kiasi gani.
Comments