top of page

NDEGE ZISIZO NA RUBANI KUSAMBAZA DAWA UKEREWE

  • Khalidi
  • Dec 15, 2017
  • 1 min read

Ndege zisizo na rubani zinatarajia kusambaza dawa katika visiwa wilayani Ukerewe lakini pia zitakuwa zinachukua sampuli mbalimbali za damu za watoto wachanga kwaajili ya kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Kanda Bugando kuazia Januari mwaka 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa maonyesho ya ubunifu wa ndege zisizokuwa na rubani.

Mongera alisema ili Tanzania tuweze kufikia nchi ya uchumi wa kati haiwezi kuiacha nyuma teknolojia hivyo ndege hizo zinatarajiwa kuwezesha kufikisha huduma ya usambazaji wa dawa katika Wilaya ya Ukerewe yenye visiwa 38 na wakazi zaidi ya 300,000.

Alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuvileta pamoja viwanda vya kutengeneza ndege zisizokuwa na rubani, Wataalamu wa afya na usafirishaji, serikali na wabunifu kuonyesha na kujifunza kitu gani kinaweza kutatua changamoto.

“Tunategemea kufikia wakati huo wadau wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani ambao wapo katika teknolojia ya juu ya kutengeneza ndege zisizokuwa na rubani.

“Wadau hao watashiriki na kufadhili hatua endelevu ya ubunifu huu, hili ni tukio la kwanza kwa Africa na nchi zinazoendelea na litatangazwa na kuitangaza Mwanza kimataifa,” alisema Mongella.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, alisema usambazaji wa dawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani utasaidia kuwahi na kutoa huduma kwa haraka na kuokoa maisha ya watu katika maeneo ambayo hayafikiki haraka.

Alisema nyingine ni uagizaji wa dawa kwa haraka na kupunguza gharama za kutunza dawa MSD kwani zitakuwa zinaingia na kutoka.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page