MLIPUKO WA AJABU WAMJERUHI MWANAFUNZI SEKONDARI DAR
- Khalidi
- Dec 15, 2017
- 1 min read

Mlipuko wa ajabu unavyodhaniwa kuwa ni matokeo ya ajali katika jaribio la kisayansi, ulimjeruhi vibaya mwanafunzi wa shule ya sekondari Fray Luis Amigo kwenye ukumbi wa PTA-Sabasaba, Dar es salaam jana na kuzua taharuki kubwa kwa watu waliokuwapo.
Mlipuko huo ulitokea mbele ya katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya elimu kwa mkoa wa Dar es salaam na kuhusisha wanafunzi wa shule mbalimbali na walimu wao.
Katika mlipuko huo, mwaanafunzi Nickson Simon wa kidato cha tatu katika shule ya fray Luis Amigo iliyoko Tungi, Kigamboni jijini Dar es salaam, alijeruhiwa vibaya katika mkono wa kulia.
Baada ya tukio hilo, mwandishi alishuhudia mwanafunzi huyo akipandishwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser VX, lenye namba STK 1664, lililokuwa limemfikisha mgeni rasmi mahali hapo na kisha kumuwahisha majeruhi huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.
Mwanafunzi huyo alikuwa jirani na meza ya wanafunzi wa shule ya sekondari Azania ambako ndiko mlipuko ulitokea wakati mgeni rasmi akipewa maelezo kutoka kwa wanafunzi kuhusiana na umeme
Comments