top of page

UTATA MAMILIONI KUNASWA AIRPORT

  • kha
  • Dec 14, 2017
  • 2 min read

Utata umeibuka kuhusiana na sababu za watu kukutwa uwanja wa ndege Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam, wakiwa na fedha taslimu za kigeni zenye thamani ya dola za Marekani milioni moja, sawa na zaidi ya bilioni 2.2.

Wizi, Utakatishaji fedha, ufadhili wa matukio haramu na upuuzaji wa sheria za nchi kuhusiana na kiasi cha juu cha usafirishaji fedha taslimu ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa chanzo cha kukamatwa kwa mamilioni hayo ya fedha, kwa mujibu wa baadhi ya wataalamu wa masuala ya fedha na uchumi.

Rais John Magufuli ndiye aliyefichua juu ya taarifa za kukamatwa kwa fedha taslimu za Marekani kiasi cha dola milioni moja. Zilikuwa zinaingizwa nchini kwa madhumuni yasiyofahamika, hivyo vyombo vya dora kuendelea na uchunguzi zaidi.

Rais Magufuli alieleza jambo hilo wakati akisisitiza benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuongeza umakini katika kusimamia masuala ya fedha. Alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa tawi la beki ya CRDB lililoko katika jingo LAPF mjini Dodoma.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya fedha na uchumi walisema kuwa kitendo hicho cha kusafirisha fedha taslimu za thamani ya kiwango cha kufikia mabilioni kinaashilia mambo mengi yanayohitaji majibu ya kina, ikiwamo hofu kuwa ni jaribio la kuingizwa nchini kwa fedha zilizopatikana kwa njia haramu.

Aidha utata mwingine kuhusishwa na fedha hizo, ni uwezekano kuwa pengine zina lengo la kufadhili matukio yanayokwenda kinyume na sheria za nchi ikiwamo ujambazi na ugaidi.

.

“Inawezekana pia wahusika hao wanamiliki fedha hizo kihalali na wala hawana nia ovu… lakini uingizwaji wa fedha taslimu za kiwango kikubwa kiasi hicho ni ukiukwaji wa sheria. Hivyo vyombo vya dola vina kila sababu ya kuendelea na uchunguzi wa kina ili kuondoa utata wa fedha hizo,” mmoja wa wataalamu wa fedha

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page