top of page

TFDA WAKAMATA BIDHAA ZILIZOZUILIWA

  • Khalidi
  • Dec 14, 2017
  • 1 min read

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), imekamata bidhaa zilizopigwa marufuku nchini zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 zikiwa zimeingizwa nchini kinyume cha sheria.

Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Charles Bujungu, alisema bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na makasha 688 ya mvinyo na 486 ya vipodozi aina tofauti yenye viambata vya sumu zilizopigwa marufuku kuingizwa nchini.

Alisema bidhaa hizo zilikamatwa eneo la Songwe mwaka Viwandani zikisafirishwa kwenye gari la Fuso lililokuwa likitokea Tunduma Mkoani Songwe kwenda Dar es salaam.

Meneja huyo alisema gari lililokamatwa na mzigo ni mali ya mfanyabiashara Yahaya Shekigenda mkazi wa Himo Mkoani Kilimanjaro ambaye alikiri gari yake kufuata mzigo wa Vinywaji mpakani Tunduma mkoani Songwe.

Bujungu alisema gari lilikamatwa kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

Meneja wa TFDA kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga alisema kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003 bidhaaa zenye viambata vya sumu zimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa na madhara ya Afya ya binadamu.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page