top of page

Rais Magufuli arudisha zaidi ya hekari 100 na kusema yeye atazikwa Chato.

  • Rehema Lucas
  • Dec 14, 2017
  • 1 min read

Utamaduni na Mila nyingi za Kitanzania huwa zinataka Mtanzania kuzikwa sehemu ya chimbuko lake. Utamaduni na Mila hii imekuwa mkombozi kwa Wananchi wa Iyumbu baada ya Rais Magufuli kutamka kuwarudishia Wananchi eneo la zaidi ya hekari mia moja ambazo zilitengwa kwa ajili ya maziko ya Viongozi.

Rais Magufuli ambae kwa mila za Kitanzania ni mtani wa wagogo alitumia maneno ya utani kufikisha ujumbe huo uliowafurahisha wakazi wa Iyumbu. “ Mimi siwezi kuzikwa Dodoma halafu mje kucheza ngoma kwenye kaburi langu”.

Rais Magufuli bila kutaja majina la marais wa zamani aliowauliza kabla ya kuamua alisema wote wanataka kuzikwa walikotoka na hata Mzee Malecela na Spika Ndugai wanatoka Dodoma lakini watataka wazikwe sehemu ya asili yao.

Je wewe msomaji wa fahari news unapenda pia kuzikwa sehemu ya asili yako au popote pale Tanzania?


Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page