top of page

MBOWE: TUME YA UCHAGUZI INAKWEPA KUKAA NA SISI MEZA MOJA

  • Khalidi
  • Dec 13, 2017
  • 1 min read

Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi (ukawa) vimeinyoshea kidole tume ya Taifa ya uchaguzi (Nec) kwa madai ya kuwanyima fursa ya kukutana mezani na kujadili changammoto zilizopo kwenye uchaguzi nchini

Mwenyekiti wa (Chadema) Freeman Mboye alisema kama tume inataka kuwapo kwa uchaguzi wenye sura ya vyama vingi ni vyema ikakubali kukaa kwenye meza moja ya mazungumzo

“Duniani kote kinachomaliza swala lenye migogoro ni mazungumzo ya meza moja lakini NEC inatukwepa bila sababu” alisema Mboye

Wakati huo aliekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii Razalo Nyalandu alitangaza kujiuzuru nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kukihama chama chake cha CCM Oktoba 30 mwaka huu kisha kujiunga na Chadema .

Ukawa iliitaka tume hiyo kuusogeza mbele uchaguzi huo wa Jimbo la Singida Kaskazini ili kwanza kuwe na majadiliano baina ya NEC na vyama vya siasi na wadau wengine wa uchaguzi kuepuka kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 uliofanyika November 26 mwaka huu ambapo Chadema ilisusia uchaguzi katika majimbo matatu

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page