LISSU APONA MAJEREHA BADO VIUNGO
- Khalidi
- Dec 13, 2017
- 2 min read

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (pichani), amesema majeraha yaliyotokana na risasi zilizoingia mwilini mwake yamepona, isipokuwa viungo.
Pia amesema siku aliyofikishwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, mwili wake ulikuwa vipande vipande baaada ya risasi 16 kuingia mwilini.
Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, mwaka huu akiwa nuje ya nyumba yake mjini Dododma, alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa na radio ya Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW).
Katika mahojiano hayo, Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), alisema siku aliyopigwa risasi, kila kiungo cha mwili wake kilikuwa kimechanika.
“Naendelea vinzuri, bado sijapona ndiomaana nipo hapa kitandani, ninaposema ninaendelea vinzuri ni kwa sababu majeraha ya risasi yamepona na kwa maelezo ya madaktari, kuna risasi 16 ziliingia katika sehemu mbalimbali za mwili wangu.
“Miezi mitatu ya baada ya lile shambulio la kigaidi, majeraha yamepona, iliyobaki ni kunifanya nitembee na kufanya shughuri zangu kama binadamu wengine. Ni safari ndefu kidogo, lakini hali yangu itarejea kama kawaida.
“Nilifikishwa hapa nikiwa vipande vipande, miguu imevunjika, mikono imevunjika na matumbo yakiwa yamechanwa chanwa, nilikuwa na hali mbaya sana sikuwa na mtu wa kuishi,” alisema Lissu.
Alisema kwasasa anaendelea vinzuri ingawa ni vigumu kurudia hali yake ya awali.
“kwa mujibu wa madaktari wanaonitibu, wanasema ni safari ndefu kurudi katika hali yangu, lakini nitarejea na kuendelea na shughuli znagu za kawaida,” alisema.
Lissu alisema kuwa mara bada ya kushambuliwa, hakuna kiongozi yeyote wa bunge aliyefika Hospitalini hapo kumjulia hali.
“Ni mwenzi wa tatu sasa Spika hajaja, Naibu wake hajaja, Katibu wala kamati inayoshughulikia hawajaja wala kunisaidia kwa namna yoyote,” alisema Lissu.
Alisema msaada huo si fadhila bali ni sheria waliyojiwekea bungeni, kuwa mbunge anapougua na kulazwa ndani au nje ya nchi, anapaswa alipwe gharama zote na Bunge.
“Hakuna sehemu ilipoandikwa ndani ya sheria za uendeshaji wa Bunge kuwa gharama hizo zitalipwa kama mbunge akitibiwa Muhimbili ama India,” alisema.
Akizungumza kuhusu kauli ya IGP Simon Sirro kuwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari na si kwa jeshi hilo, Lissu alisema jeshi hilo linanamna nyingi za kupata taarifa.
Alisema maisha yake yote atayatumia katika haki kwani anayedai haki ni mpenzi wa mwenyezi mungu.
“Nasubiri nipone kama ambavyo madaktari wamesema nitasimama nitatembea na nitaendelea kudai haki kwa kuwa maandiko yanasema haki huinua taifa,” alisema Lissu
Comments