SIRI YA POLISI KUBAKI KIBITI.
- Khalidi
- Dec 11, 2017
- 1 min read

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Sirro jana alieleza siri ya askari wake kuendelea kuwapo katika wilaya ya Kibiti mkoani Pawni licha ya eneo hilo lililokuwa limegubikwa na mauaji mfurulizo ya watu wasio na hatia kutulia kwa muda mrefu.
IGP Sirro ambaye ukomeshaji wa mauaji ya raia pwani ilikuwa moja ya ahadi zake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo Mei 29, mwaka huu, alisema polisi inaendelea na operesheni ya usalama katika eneo hilo ili kutokomeza kabisa uhalifu uliokuwa ukifanyika.
Alisema kwasasa Kibiti ni shwari lakini Jeshi la polisi linaendelea na operesheni kuhakikisha mauaji yaliyoigubika kwa zaidi ya mwaka mmoja hayatokei tena.
Watu 40, wakiwamo askari polisi 15, walilipotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi Kibiti na Wilaya za Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani tangu mauaji hayo yalipoanza mwaka 2015.
IGP Sirro alisema baadhi ya wahalifu kutoka maeneo hayo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji walikuwa wamekimbilia mkoani humo na kwamba askari wake walikuwa wakiendelea kuwasaka kwa nia ya kupambana nao.
Alisema hakuna sababu ya mtu yeyote kuhofia kwasababu usalama upon a mauaji yamekwisha.
IGP Sirro alisema lengo la polisi ni kuona wakazi wa kibiti wanaishi bila hofu yoyote kutokana na ulinzi kuimarishwa na kwamba jeshi lake lipo imara na limefanikiwa kudhibiti uhalifu uliokuwa katika eneo hilo.
Comentarios