top of page

KILI STARS KUREJEA NYUMBANI USIKU WA LEO

  • Rehema Lucas
  • Dec 11, 2017
  • 1 min read

kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) kinatarajia kurejea nyumbani leo usiku baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya.

Kilimanjaro Stars inarejea nyumbani baada ya kufanya vibaya katika hatua ya makundi na kushindwa kutinga katika hatua ya nusu fainali huku wakiwaacha ndugu zao zanzibar Heroes wakiendelea na michuano hiyo.

Zanzibar itakutana na mabingwa watetezi, Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya, Desemba 15, mwaka huu.

Hiyo itakuwa nusu fainali ya pili, baada ya nusu fainali ya kwanza kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Burundi mchezo huo utachezwa Desemba 14.

Katika mchezo wa leo dhidi ya Kenya, Tanzania bara imepoteza mchezo wa tatu mfululizo kwa kufungwa bao moja kwa sifuri na kumaliza kwenye nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A


Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page