JWTZ YASIKITISHWA NA VIFO VYA WANAJESHI 14 VILIVYO TOKEA CONGO
- Rehema Lucas
- Dec 11, 2017
- 1 min read

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na kitendo cha waasi walio julikana ni ADF kuvamia Kikundi cha ulinzi na usalama kilichopo DRC kwaajili ya kutekeleza jukumu la ulinzi na amani nchini humo na kusababisha Mauaji kwa askari 14 wa Tanzania.
Akithibitisha mauaji hayo muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema shambulio hilo la kuvamiwa lilizusha mapigano baina ya kikundi cha askari wa Tanzania na kile chwa waasi na yalidumu kwa takribani masaa kumi na tatu na kusababisha vifo vya askari wa Tanzania 14 na wengine 44 kujeruhiwa na askari wawili hawajulikani walipo ambapo jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Ameongeza kuwa shambulizi hilo la tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Desemba lilikuwa ni shambulizi baya na halijawahi kutokea tangu vikosi hivyo vianze kushiriki ulinzi wa amani nchini DRC mwaka 2011,hata hivyo kikundi hicho ambacho bado kipo huko kinauwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu husika kwa uhodari wa hali ya juu,ushupavu,weledi mkubwa na umahiri stahiki.
Aidha amesema taratibu za kuisafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini zinafanyika chini ya utaratibu wa Serikali, Umoja wa mataifa na JWTZ wanaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatia tukio hilo ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika sambamba na kuangalia taratibu za kuwajulisha familia za wafiwa zimekamilika na ndio maana hawakuweza kutoa taarifa hizo bila kuwaweka sawa familia za mashujaa hao.
Mwakibolwa amewataka Watanzania kwa Umoja kuwaombea dua roho za mashujaa hao zipumzike kwa amani na majeruhi wote wapone haraka ili warejee kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ulinzi wa taifa na dunia nzima
Comments