top of page

HATUA YA MAKUNDI CECAFA CHALLENGE CUP KUKAMILISHWA LEO KWA MICHEZO MITATU

  • Rehema Lucas
  • Dec 11, 2017
  • 1 min read

Hatua ya makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge inayoendelea nchini Kenya, inatarajiwa kukamilishwa leo kwa michezo mitatu.

Saa 8:00 mchana, Zanzibar watamenyana na Libya Uwanja wa Jomo Kenyatta, Machakos mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Tanzania Bara Saa 10:00 jioni, zote zikiwa mechi za Kundi A, wakati Uwanja wa Kakamega kutakuwa na mchezo mmoja wa Kundi B kati ya Sudan Kusini na Burundi kuanzia Saa 9:00 Alasiri.

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje ambaye amesema hataki kuondoka Kenya na pointi moja pekee bali angalau washinde na kupata pointi nne.

Kilimanjaro Stars itaendelea kuwakosa beki wa kati Kelvin Yondan ambaye bado ana maumivu ya kifundo cha mguu na Mbaraka Yusuph aliyepata majeraha ya misuli.

Kilimanjaro Stars ipo mkiani mwa Kundi A wakiwa na pointi moja waliyoipata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Zanzibar wanaongoza kundi hilo A wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Kenya wenye pointi tano, Rwanda wenyewe wana pointi nne wakati Libya wana pointi tatu na katika Kundi B ni Uganda na Burundi zinazoelekea kwenda Nusu Fainali.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page