FAMILIA YAMFUNGA MDOMO BABU SEYA
- Khalidi
- Dec 11, 2017
- 2 min read

Familia ya Mwanamziki Nguza Viking maarufu kama ‘Babu Seya’ imeamua kumzuia yeye na Mwana Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ Kuzungumza na vyombo vya habari hadi katikati ya wiki.
Babu Seya na Papii waliachiwa huru saa 12:08 jioni baada ya Rais DK. John Magufuli kuwapa msamaha.
Mwanamziki ambaye yuko karibu na familia hiyo, Nyoshi EI Sadaaty alisema amefanya uamuzi huo kuwapa muda wa kutosha kupumzika.
Alisema kutokana na kuwa na hali ya uchomvu na mshangao huenda wakazungumza mambo ambayo hawastahili kuyazungumza .
“Familia iliamua wasizungumze na vyombo vya habari hadi Jumanne au Jumatano ili wapumzike na wajipange cha kuzungumza kwa jamii,” alisema Nyoshi.
Alisema kwa sasa Babu Seya na Papii wako katika nyumba yao mpya ya Tegeta ambayo walinunua baada ya kuuza ile ya Sinza.
“Nguza na Papii ako Tegeta kwa sasa lakini Familia iko Kimara Stopover ambako nako walinunua nyumba,” alisema Nyoshi.
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wengi, juzi Babu Seya na Papii hawakuzungumza chochote bali waliingia katika gari dogo la rangi ya fedha na kwenda katika Kanisa la Life Christ Ministry lililopo Segerea mwisho jijini Dar es salaam ambako mtoto wake aliyeachiwa huru mwaka 2010 Nguza Mbangu ni mchungaji.
Walipofika hapo waliingia na kupiga picha kabla ya kuondoka huku wakiomba waachwe wapumzike na kuahidi kuzungumza jana.
Akihutubia juzi katika kilele cha sherehe za miaka 56 ya Uhuru mjini Dodoma, Rais Magufuli alisema ameamua kutekeleza kwa vitendo Ibara ya 45 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema:
“Bila kuathiri masharti mengine katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Rais anaweza kutenda lolote ili mtu huyo asitimize adhabu hiyo wakati wa muda maalumu.
“C. kulinganisha adhabu na tahfif waswahili wanajua tafsiri yake vinzuri kina Kikwete (Rais wa awamu ya nne) sisi wa bara ni ngumu.
“Ibara hii pia ninatoa msamaha kwa familia ya Nguva Viking jina jingine Babu Seya na mwanae Johnson Nguza ‘Papii Kocha, nao waachiwe huru,” alisema Rais Magufuli.
Alisema wafungwa waliohukumiwa kifungu cha maisha ni 666 kati yao` wanaume ni 665 na wanawake ni 11.
Comments