DC AAGIZA TAKUKURU IICHUNGUZE ACACIA
- Khalidi
- Dec 11, 2017
- 1 min read

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara. Glorious Luoga, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani humo,kuichunguza ofisi ya kitengo cha mahusiano katika Mgodi wa Acacia North Mara baada ya kubaini udanganyifu wakati wa kusaidia wajasiliamali.
Luoga alitoa agizo hilo baaada ya kukutana na vikundi vya wajasiliamali vilivyoko Nyamongo, ambapo baadhi ya wajasiliamali walionyesha kutokuwa na imani juu ya misaada wanayopokea kutoka katika mgodi huo.
“Katika taarifa niliyoisikia hapa, kuna fedha nyingi zinaonyesha zimepelekwa kwenye miradi ya hivi wakati kiuhalisi ni uongo, yaani ni danganya toto. Kwahiyo, nawataka Takukuru mfanye uchunguzi kasha mlete majibu mapema,” aliagiza Luoga.
Kwa mujibu wa Ojendo, Mgodi wa Acacia North Mara umekuwa msaada kwa jamii inayouzunguka na umekuwa ukiwasaidia katika Nyanja mbalimbali japokuwa changamoto haziwezi kukosekana.
Comments