top of page

AGIZO JPM LALETA UFANISI BANDARINI

  • Khalidi
  • Dec 11, 2017
  • 2 min read

Agizo la Rais John Magufuli la kuitaka Mamlaka ya Huduma za bandari (TPA) kutoa huduma kwa saa 24 limesaidia kupunguza mrundikano wa mizigo bandarini na kuibua malalamiko kutoka kwa watumiaji wa bandari.

Hayo yalibainishwa na wadau wakati wakizungumza mwishoni mwa wiki katika kipindi cha ‘kipimajoto’ cha runinga ya ITV.

Katika kipindi hicho ambacho mada ilikuwa ‘utaratibu wa Bandari kufanya kazi kwa saa 24 kwa siku je, umesaidia kuongeza kasi ya kutoa mizigo,” walisema agizo hilo mbali na kupunguza mrundikano wa mizigo, pia limeleta ufanisi katika huduma za bandari.

Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama, alisema agizo la rais limesaidia kasi ya kuondoa mizigo kwa kuwa limehusu taasisi zote zinazotoa huduma bandarini. Alisema awali TPA ndiyo ilikuwa ikitoa huduma muda wote, lakini agizo hilo limegusa taasisi zote kutoka huduma muda wote, kuazia wenye mizigo, Mamlaka ya mapato (TRA), mawakala wa meli na zingine.

Alifafanua kuwa agizo la Rais Magufuli lilitolewa baada ya kupitishwa na kusainiwa kwa mapendekezo ya kuzitaka taasisi zote kutoka huduma kwa saa 24, mwaka 2009, limesaidia kuongeza pia ushirikiano na ushirikishwaji miongoni mwa wadau.

“Pia taasisi za kibenki zimepewa fursa na TPA kuweka benki zao ndani ya bandari, bila hivyo tungekuwa katika kipindi cha hali ya mrundikano cha mwaka 2008/2009,” alisema..

Katika kipindi hicho ambacho mada ilikuwa ‘utaratibu wa Bandari kufanya kazi kwa saa 24 kwa siku je, umesaidia kuongeza kasi ya kutoa mizigo,” walisema agizo hilo mbali na kupunguza mrundikano wa mizigo, pia limeleta ufanisi katika huduma za bandari.

Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama, alisema agizo la rais limesaidia kasi ya kuondoa mizigo kwa kuwa limehusu taasisi zote zinazotoa huduma bandarini. Alisema awali TPA ndiyo ilikuwa ikitoa huduma muda wote, lakini agizo hilo limegusa taasisi zote kutoka huduma muda wote, kuazia wenye mizigo, Mamlaka ya mapato (TRA), mawakala wa meli na zingine.

Alifafanua kuwa agizo la Rais Magufuli lilitolewa baada ya kupitishwa na kusainiwa kwa mapendekezo ya kuzitaka taasisi zote kutoka huduma kwa saa 24, mwaka 2009, limesaidia kuongeza pia ushirikiano na ushirikishwaji miongoni mwa wadau.

“Pia taasisi za kibenki zimepewa fursa na TPA kuweka benki zao ndani ya bandari, bila hivyo tungekuwa katika kipindi cha hali ya mrundikano cha mwaka 2008/2009,” alisema.

Comentarios

Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page