ALIYEKUWA MKURUGENZI WA NKASI AHOJIWA TAKUKURU
- Rehema Lucas
- Dec 10, 2017
- 1 min read

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Rukwa inamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi na Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Kaondo, ikiwa ni hatua za kukusanya ushahidi wa kutosha dhidi ya tuhuma anazokabiliana nazo.
Kaondo anatuhumiwa kukiuka taratibu za manunuzi hivyo kuisababishia Serikali hasara kubwa ya zaidi bilioni saba.
Hatua hii inafuatia maagizo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa My Selemani Jafo baada ya kusimamisha kazi.
Comments