top of page

Rais Magufuli anogesha Sherehe za Uhuru kwa kuwaachia huru Babu Seya na Papii Kocha

  • Robert Lazaro
  • Dec 9, 2017
  • 1 min read

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo katika sherehe za Uhuru zinazofanyika mkoani Dodoma ameamua kuwasamehe Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha) kuanzia leo.

Katika msamaha huo pia Rais ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 huku 1828 kuachiwa huru kabisa na 6329 watapunguziwa muda wao wa kukaa gerezani.

Katika msamaha huo pia Rais Magufuli amewasamehe wafungwa 61 ambao hukumu yao ilikuwa ni kunyongwa na hivyo wahusika wafanye mchakato kwa ajili ya kuwaachia huru Leo na kesho.


Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page